Sunday, November 25, 2007

Uganda: Aibu yaikumba upinzani

Wiki jana Kampala, Uganda, ilijaa na wageni kutoka nchi 52 zilizoko katika jumuiya ya nchi za madola.


Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza alikuwa mgeni wa heshima katika mkutano huo.

Cha kustajaabisha ni vile vyama vya upinzani badala na kufanya wageni wahisi nyumbani waliamua kufanya migomo. Serikali ya Uganda iliwapa ruhusa kufanya mgomo katika kiwanja cha ndege cha Kololo lakini vyama vilipuuza na kuamua kuingia jijini.

Polisi wa kizima ghasia hawakusita kuwacharaza waliovunja sheria.

Kulingana na mimi, badala ya kufanya migomo viongozi wa upinzani wakijiandaa kupatana na Malkia na wageni kutoka mataifa mengine, aghalabu waelezee matatizo ya kwa njia ya kistaarabu.

Pole sana upinzani kwa kukosa mwelekeo na sijui kama mtapata nafasi ya kunena na wageni tena.

Ukidhani ni vyama vya upinzani tu vilivyogoma utakuwa umekosea. Wafalme wa Buganda na Bunyoro walidinda kupatana na Malkia Elizabeth wakidai kwamba ni lazima wasuluhishe madhambi ambayo Uiengereza ilifanyia falme hizi.

Swali kwa falme hizo, Malkia Elizabeth alikuwa wa wadhifa alio nao wakati madhambi yalikuwa yakifanyika? Je, falme zingepeleka kesi zao kati mahakama ya kimataifa, siwangepata suluhu?

Picha/timesonline.co.uk

Thursday, November 22, 2007

Kuna umuhumu wa mkutano wa nchi za madola?

Mkutano wa nchi za madola unaofanyika Uganda ni jambo la kufurahisha sana.

Malkia Elizabeth wa pili wa Uiengereza yupo Kampala na kando na kuongoza mikutano muhimu atazuru kituo cha HIV na Ukimwi cha Mildmay na mbuga ya Queen Elizabeth.


Je, mkutano wa nchi za madola ina umuhimu wowote??

Friday, November 09, 2007

Kuawa na kuvuutwa kwa maiti ya wanajeshi waethiopia

Mwaka wa 1993 wanajeshi wa marekani walipouawa na kuvurutwa katika mitaa ya Mogadishu ilikuwa ni onyo na wengi walidhani ni mara ya mwisho kwa visa kama hivyo kufanyika.

Wiki hii, wanajeshi watatu wa Ethiopia waliuawa na waasi, kisha maiti zao kuvurutwa kinagaubaga katika mitaa ya Jiji la Mogadishu huku waasi hao wakishangilia wakisema "mungu ni mkubwa."

Je, hii ni kusema wasomali wenye msimamo mkali wamechoka na majeshi ya Ethiopia?, Hii ni kusema wanajeshi wa Ethiopia wameshindwa katika kuithibiti na kuilinda Mogadishu?, Je, hii ni inadhihirisha wanasomali/ waasi wanawaambia wanajeshi waethiopia waondoke Somalia??

Picha/Associated Press

Monday, November 05, 2007

Kenyana









Wakati ni huu kusikia
Wakati ni huu kufikiria
Ni nani wa kupigia kura?

Yachukua muda kuchagua
Je, ni yule mwenye uwazi?
Je, ni yule mwenye kweli?

Si semi mpigie nimpendaye
Nasema fungua macho
Amua nani kiongozi wako

Chagua vyema Kenyana
Jua kura yako ni nguvu
Bila wewe hawawezi

Baada ya kura…kenyana
Asipotimiliza matakwa…
Kura yako ni ufagio
Katiba ni ngao

Kenyana piga KURA