Thursday, August 30, 2007

Ukimwi : Mbona Vijana tena


Wiki moja iliyopita nilikuwa katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Mildmay (The Mildmay Centre) katika hoteli ya kifahari ya Sheraton, jijini Kampala.

Mildmay iliona ni muhimu kuwa na mazungumzo na waandishi, wahariri na waratibu vipindi kutoka vituo mbalimbali vya habari ilikubuni mbinu ambazo zitawezesha kuripoti na uchapishaji wa habari kuhusu ugonjwa wa ukimwi.

Kwa ufupi Mildmay ilijitolea kuwafunza waandishi wa habari mengi kuhusu ugonjwa wa ukimwi na waandishi wa habari wakajitolea kuripoti habari muhimu na kufunza umma.

Papo hapo, nilifanikiwa kupatana na wahudumu wawili kutoka kituo cha Mildmay na tukaanza kunena kuhusu vyanzo vya vijana kupata ugonjwa wa Ukimwi.

Tulitaja mambo kama ukosefu wa mafunzo ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huo, kubusu kwa undani mwenye ukimwi ilhali mbusu ana vidonda mdomoni, kutumia makali kama sindano na wembe kwa pamoja na mtu aliyeugua ugonja huo, ukosefu wa uaminifu katika uhusiano na kufanya ngono (usherati au uzinzi). Lakini kuna jambo moja ambalo waligusia na ikanishtua.

Jambo hilo ni, kuwa watu wengi walioelimika au wanafunzi wanapata ugonjwa wa ukimwi si eti ni kwa sababu hawana habri kuhusu ugonjwa huo unavyosambaa na kupatwa, lakini ni kwa sababu wanapuuza habari hiyo na kudhani waliosoma hawawezi kuupata ugonja huo.

Je, sababu hii tutaipiga vita?