Ukimwi : Mbona Vijana tena
Wiki moja iliyopita nilikuwa katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Mildmay (The Mildmay Centre) katika hoteli ya kifahari ya Sheraton, jijini
Mildmay iliona ni muhimu kuwa na mazungumzo na waandishi, wahariri na waratibu vipindi kutoka vituo mbalimbali vya habari ilikubuni mbinu ambazo zitawezesha kuripoti na uchapishaji wa habari kuhusu ugonjwa wa ukimwi.
Papo hapo, nilifanikiwa kupatana na wahudumu wawili kutoka kituo cha Mildmay na tukaanza kunena kuhusu vyanzo vya vijana kupata ugonjwa wa Ukimwi.
Tulitaja mambo kama ukosefu wa mafunzo ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huo, kubusu kwa undani mwenye ukimwi ilhali mbusu ana vidonda mdomoni, kutumia makali kama sindano na wembe kwa pamoja na mtu aliyeugua ugonja huo, ukosefu wa uaminifu katika uhusiano na kufanya ngono (usherati au uzinzi). Lakini kuna jambo moja ambalo waligusia na ikanishtua.
Jambo hilo ni, kuwa watu wengi walioelimika au wanafunzi wanapata ugonjwa wa ukimwi si eti ni kwa sababu hawana habri kuhusu ugonjwa huo unavyosambaa na kupatwa, lakini ni kwa sababu wanapuuza habari hiyo na kudhani waliosoma hawawezi kuupata ugonja huo.
2 Comments:
Kweli kabisa kuna watu wengi ambao wanajua ni nini kitawasababisha waambukizwe UKIMWI ila bado wanafanya hayo mambo. Siamini kuwa watu walioelimika hutenda kwa kufikiria kwa sababu wameelimika hawata pata virusi. Naamini huwezi kujiita umeelimika halafu ukafanya jambo liashirialo kuwa hujaelimika kwa kisingizio kuwa umeelimika ndio maana unafanya hivyo.Naamini watu hawa hufanya kwa kuwa hawajali na pia wanakautulivu kakujidanganya kuwa kuna kaasilimia fulani kuwa wafanyaye nao ngono hana vijidudu. Wanacheza bahati nasibu ya virusi.
kitururu apo unasema wengi! duh!sichangii
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home