Wednesday, June 25, 2008

Suluhu ya njaa barani ni ipi?

Siku zinayoyoma huku nambari ya watu wanaoaga kutokana na njaa katika pembe ya Afrika yaongezeka. Somalia imehadhirika zaidi kutokana na upungufu wa mvua na machafuko ya kivita inayozuia ugawanyaji wa chakula.

Takwimu za umoja wa mataifa (UN) zaonyesha watu milioni 14.5 million wanahitaji msaada wa kibinadamu kwa haraka. Idhaa ya BBC inaripoti kuwa watoto wengi wanautapiamlo.

Ripoti hizi zinauzito mwingi sana, lakini mbona ulimwengu haukimbii kuinisuru Somalia? Jibu kwa swala la upungufu wa chakula barani ni nini ilhali Afrika ni kikapu cha chakula ulimwenguni?

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home