Tuesday, September 04, 2007

Nipe Bunduki!!

Kipindi cha 'World Have Your Say (WHYS)' kwenye idhaa ya BBC, Ijumaa iliyopita, kati ya mada zilizojadiliwa, moja yao ilikuwa ni 'Jamii yenye silaha ni jamii karimu.'

Chanzo ya mada hii ni wazo la mshiriki mmoja aliyetaja alhamisi kuwa, “Kisa Virginia Tech ingekuwa na uzito mdogo iwapo wanafunzi wangejua jinsi ya kutumia bunduki.”

Mada hiyo ilinilazimisha kurusha macho yangu Afrika ninakoishi. Fikra zilisonga:

Je, kwa nini waja barani wafunzwe bunduki, ilhali wachache wajuao wanatuhangaisha?

Je, nikijua bunduki nitaangamiza visa vya uporaji, uasi, nitawalinda wanyanyaswa hasa watoto na mabinti/akina mama? Kazi ya polisi itakuwa gani?

Je, hasira ikinipanda nitaweza kufanya uamuzi mzuri palipo na tatizo?

Je, kuna nchi au polisi wataweza kusitisha ghasia wananchi wakibeba silaha?

Ndugu zanguni nisaidieni, Bara la Afrika itakuwa bora kabisa wewe na mimi tukijua kutumia bunduki na kuimiliki?

1 Comments:

At 2:26 PM , Blogger Simon Kitururu said...

Nafikiri hakuna tatizo katika kujua jinsi ya kutumia bunduki. Tatizo linakuja tu katika umiliki wa silaha wakati hali zetu mpaka siasa zetu hazieleweki

 

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home