Tuesday, January 08, 2008

Sauti

Thursday, January 03, 2008

Kenya ina kilio

Kenya ina kilio,
Kwani mwai Emilio,
Aliyepata kura chache millioni,
Alipojiapisha rais,
Uhasama fujo ikajaa,
Maisha hayakuwa raisi,
Damu damu mitaani,
Hadi wakenya wanapoishi,
Polisi jeshi na askari jeshi t-w-a t-w-a,
Wakaua wananchi wenzao,
Waliokuwa wakipigania haki zao,
Je, polisi hawa wana koo zao?
Je, wanaelewa demokrasia?
Wanamtumikia nani?
Taifa au rais?


Ukabila ukajikita,
Wasio wa kabila hili wakafukuzwa,
Wa kabila lile wakauawa,
Mali ya kabila hilo yakachomwa,
Hata watoto wakaangamizwa kanisani, Eldoret,
Je, kabila ni bora kuliko ukenya?
Nani hana haki ya kupigia kura atakaye?
Kura ni siri, ulijuaje aliyepigia kura?
Mbona hasira kwa asiyekuwa tume ya uchaguzi?


Uchungu na chuki, Usoni mwa wakenya,
Si fikiri majimbo sasa,
Ipeni miongo miongo,
Lakini…si mwanako ameoa kutoka jamii ile?
Ah…mamangu ni kutoka pwani,
Ah…babu yangu anatoka Iten na Wajir,
Pole pole…elimu ya uzalendo kwanza,
Pia ichukue muda,


Kenya tupendane na tufanye haki.