Wednesday, November 08, 2006

Waambaji chakita mizizi

Mwaka huu ulianza na ufinyo mkubwa wa kuhakikisha lugha ya kiswahili kinatumiwa kote huku Uganda. Chanzo hasa, ni uanachama wa Uganda katika Jumiya ya Afrika Mashariki, ambao uliilazimisha Uganda, kuharakisha mikakati ya kukieneza Kiswahili ilikurahisisha mawasiliano na mwingiliano kati yake na nchi za jumuiya zikiwepo Kenya na Tanzania.

Katika Chuo cha Makerere, Radio ya Chuo yaani 107 Campus FM, ilianzisha kipindi cha Waambaji ili kufunza Kiswahili wasikilizaji wake hasa wanafunzi, wakufunzi na wafanyikazi wa chuo. Kipindi hicho kinachorushwa kila Jumatatu saa kumi hadi saa kumi na moja za jioni, bado kinaangazia mambo kadha wa kadha katika lugha ya Kiswahili.

Jumatatu hii, 04/09/2006, Nahodha wa kipindi cha Waambaji Bw. Etale Fanuel alimwalika Bw. Ndanda Antonio na mada ya kipindi ilikuwa ni "Mikakati ya Kukiimarisha kiswahili nchini Uganda."

Kwa kukianza kipindi swali lilikuwa ni, " Je ni vyema kuidhinisha Lugha ya Kiswahili katika shule za misingi?" Bw. Etale aliuiza,

"Naam, ni vyema kukiidhinisha lugha ya Kiswahili katika shule za misingi hapa Uganda kwani muingiliano na mawasiliano katika kanda ya Afrika Mashariki inalazimu. Hivi sasa tuna Jumuiya ya Afrika Mashariki inahitaji kiswahili kama lugha kuu katika kuifanikisha Jumuiya katika mipango yake na kuendesha mambo yake. Kumbuka nchi ya Kenya na Tanzania wanazungumza kiswahili, basi Uganda ni lazima izungumze," Bw. Ndanda alijibu.

Nchini Tanzania, Kiswahili kimepewa kipao mbele na kutumiwa kama Lugha ya kitaifa na lugha rasmi. Shule, Vyuo na Afisi mbali mbali zinatumi lugha hii. Jirani yetu, Kenya pia inatumia Kiswahili kama lugha ya taifa na kunajitihada kukifanya lugha rasmi. Uganda je?

Utandawazi inatulazimu kufunza lugha hii katika shule za msingi na Uganda kwa ujumla. Biashara kati ya nchi zetu hivi sasa yahitaji aghalabu kukijua kiswahili ilikuelewa yanayotendeka kwa jirani zetu na nchi zingine.

Kiswahili bado kinafungua milango ya ajira katika kanda ya Afrika Maskariki kwa Wanauganda wanalio na bahati ya kukisoma, kukiandika, kuelewa na kikisema Kiswahili. Kwa mfano, katika vyombo vya habari, ualimu na afisi nyinginezo za afisi kama uhazili.

Ili Uganda inufaike kotakana na lugha ya kiswahili ni lazima mikakati ifuatayo kitiliwa maanani:-

  • Kutambiliwa kwa kiswahili kama moja wapo lugha rasmi na lugha ya kitaifa.
  • Kukifunza kiswahili katika shule za mchekecheo, msingi, upili, shule za ualimu na vyuo vikuu.
  • Kuzingatia kiswahili sanifu.
  • Ujira bora kwa wasemaji wa kiswahili hasa waalimu ilikuwatia motisha kikifunza.
    Uchapishaji vitabu na utafiti wa lugha ya kiswahili.
  • Utumiaji wa kiswahili katika vyombo vya habari kama vile Redio, Runinga, magazetini na jarida mbali mbali.
  • Kuandaliwa kwa mijadala, warsha, vikao na kadhalika.

Ingawa mikakati ya kukiimarisha kiswahili ni nyingi mno, matatizo yanayoikumba hii ya kiswahili hayawezi kusaulika. Wanauganda wengi wana mtazamo asi dhidi ya lugha ya kiswahili. Mtazamo huo unamizizi tangia jadi eti kiswahili ni lugha ya wanajeshi, askari polisi, mabawabu na wezi.

Upungufu wa waalimu katika viwango vyote na ukosefu wa vitabu vya kiswahili hapa nchini Uganda, umetatiza kuenea na kutumika kwa lugha ya kiswahili.

Umesikia Uganda inavyoamua kutoka mavumbini na kukikuza kiswahili. Mpenzi msomaji, jiunge kikitumia kiswahili uliko. Hii ni lugha nzuri.

Kiswahili oyee !! kiswahili oyee!!