Sunday, July 29, 2007

Fichuzi yagutuka

Asalam aleikum? wasomaji wa blogu hii. Nawasabahi kwani imekuwa muda mrefu tangu nichapishe habari kati blogu hii. Shughuli zilikuwa zimenifika kooni. Natumai mmekuwa salama kwa hali na mali. Shukrani kwa wote waliojaribu kujua niliko KISIKI au wasomaji wa FICHUZI.

Mnavyojua, nia ya blogu hii ni kushughulikia maswala mbali mbali na kuwa na mtazamo tofauti au kutia changamoto kwa walimwengu na kufikia suluhu kwa pamoja.

Nakusihi kuchangia katika makala nitakayo chapisha. Kumbuka si lazima ukakubaliane nami ili kuchangia. Sisi kama walimwengu tunasaidiana tu katika unyooshaji wa mawazo au dhana.

Kwaheri kwa sasa na kumbuka Kiswahili ni lugha yako na kuwa wewe ni raia wa ulimwengu na lazima kujali kuhusu wenzako.