Thursday, July 06, 2006

Kuzidi Kony?

Ilikuwa ni jana tarehe 29/06/06, Bw. Kony aliposema ni mara ya kwanza kunena na mwandishi wa habari. Matamshi yake hayo, yanaleta utata kuhusu waandishi wengi waliodai kuwahi kuongea na Kony hapo awali.

Akihojiwa kwenye Radio ya BBC, alipoulizwa kuhusu mauaji na dhuluma aliyosababisha Kaskazini mwa Uganda, Kony anajibu kwa kimombo kilichoadhirika kwa lugha ya acholi, "Sio kweli. Siwezi kukata sikio la ndugu yangu; Siwezi kuua jicho la ndugu yangu. Siwezi kuua ndugu yangu, hiyo si kweli." [This is not true. I cannot cut the ear of my brother; I cannot kill the eye of my brother. I cannot kill my brother, that is not true.]

Kwenye matamshi hapo juu, Bw. Kony anajaribu kusahau aliyomwambia mmoja wa wale aliyekuwa ameteka kama ilivyonukuliwa na tovuti ya BBC website (http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/3462901.stm ) "Kama watu wa acholi hawataniunga mkono, ni lazima wamalizwe." [If the Acholi don't support us, they must be finished.]

Mara hii, Kony anajitetea kuwa madai ya waasi wa L.R.A (Lord Resistance Army) kukata ndimi za watu na kuwateka watoto ni propaganda ya serikali ya Uganda.

Ni miaka ishirini sasa, tangu Kony aanze uasi, ilikuona sheria kumi za biblia zinatumiwa Uganda. Lakini ni amri kumi zipi ambazo Kony anataka zitumiwe Uganda? Je, ni zile zilizoko kwenye biblia au ni vile anavyoelewa yeye mwenyewe? Hili ni kumbusho tu, kuhusu wanajihadi au 'al qaeda' wanaojaribu kuona "sharia" inatumika kote kisha waishia kuwaua wasio na hatia.

Rais Museveni amempa Kony hadi mwisho wa mwezi Julai kumaliza vita na anasema usalama wake utakua hakika. Je, usalama upi Rais Museveni anaongelea hapa, je, ni kumkabidhi kwa mahakama ya kimataifa huko Hague? Je, mwisho wa Julai ikifika na Kony asikomeshe uasi, nini kitafanyika?

Kony hamwamini Kony, vilevile Museveni hamwamini Kony. Ni kweli Kony ana uoga hakuna makao mema yakuendeleza ugaidi na anahisi hivi karibuni hatakuwepo tena. Hii ndiyo sababu ameiuliza serikali ya Sudan Kusini kuongoza mapatanisho ya amani kati yake na serikali ya Uganda. Kony anaongeza kusema ya kuwa anania ya kukomesha vita.

Kwa hivyo, kuna maswali ambayo hayajajibiwa tunavyolenga mapatanisho ya amani na Kony: Ni nani amekuwa akifadhili Kony Kaskazini mwa Uganda na hata katika nchi zingine? Nani humpa silaha? Wafadhili wake watafikishwa mahakamani? Je, watu kutoka kaskazini mwa nchi watarejelea maisha ya kawaida kijamii na hata kisaikolojia? Serikali ya Uganda itafanya nini baada ya maswala ya Kony Kukwisha? Je, Mahakama ya Kimataifa ikikana msamaha kwa Kony kutoka kwa Museveni?