Sakata ya kiongozi wa Lord Resitance Army (LRA), Joseph Kony kutosaini mkataba wa amani inaonekana kuwa shtuo kwa wanauganda, raia na viongozi wa pembe ya Afrika.
Kony anataka kufafanuliwa vipengee kadhaa katika mkataba, na amewaomba viongozi wa kitamaduni na wa dini kumsaidia.
Wiki jana, David Matsanga mjumbe mkuu katika mazungumzo ya amani kati LRA na serikali ya Uganda huko Juba, Sudan Kusini alijiuzulu. Matsanga alidai hana umuhimu kwa sasa kwani alishindwa kumbembeleza Kony kusiaini mkataba.
Wiki hii Kony alimwapisha Jame Obita kama kiongozi wa wajumbe wake katika mazungumzo ya amani. Jambo ambalo lilikaribishwa mno na serikali ya Uganda.
Je, nini kinamzuia Kony kusaini mkataba?
Kony anahofia kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya jinayi (ICC). Kwa sasa hana uhakikisho kwamba atahukumiwa katika makama za Uganda. Akirusha mawazo yake, anamwona Charles Taylor wa Liberia kizimbani huko Hague. Akilala, anamwona Slobodan Milosevic wa Kosovo kizimbani.
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni kusema Kony awezi kufikishwa Hague haipendezi, kwani waranta ya Kony kushikwa na kufikishwa ICC ipo.
Kwa muda sasa, ni wazi kwamba Kony hamwamini yeyote yule. Tunakumbuka vifo alivyovisababisha kwa manaibu waki, kama vile, Vincent Otti na Okot Odhiambo.
Kwa kifupi, Kony ataweza kusaini mkataba wa amani utaomaliza vita vilivyodumu kuzidi miaka ishirini, iwapo atahakikishwa hatafikishwa Hague.